#HABARI: Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe#HABARI: Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe

#HABARI: Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, ameeleza kuwa jumla ya vitongoji 1,997 sawa na asilimia 88.4 kati ya vitongoji 2,260 vimeshapatiwa huduma ya umeme kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), iliyopita na inayoendelea kutekelezwa katika mkoa wa Kilimanjaro.

Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amebainisha hayo wakati wa ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, sambamba na kuzungumza na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA ambapo ameweza kushuhudia wananchi wakiunganishiwa huduma ya umeme Wilaya ya Hai mkoani humo.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania #uchaguzimkuu2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *