
Nchini Senegal, mamlaka zinarahisisha hali kwa familia za wale waliouawa wakati wa maandamano ya kabla ya uchaguzi kupokea faranga za CFA milioni 10 zilizoahidiwa na mamlaka mpya. Kulingana na serikali ya Senegal, familia za watu 74 waliofariki wakati wa machafuko ya kisiasa kati ya mwezi wa Februari 2021 na 2024 wanahsika na hatua hii.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff
Tangu mwisho wa mwezi wa Januari na kutangazwa kwa usaidizi wa kifedha, waathiriwa wa maandamano ya kabla ya uchaguzi nchini Senegal—watu 1,931 waliozuiliwa isivyo haki kulingana na mamlaka mpya—wamepokea kila mmoja faranga za CFA 500,000. Watu mia moja na ishirini na saba waliojeruhiwa wamepokea msaada wa matibabu, Wizara ya Familia na Mshikamano imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Lakini ni familia za watu 66 waliouawa wakati wa maandamano haya, kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International (80 kwa mujibu wa mamlaka), ambao wamekwama… Suala ni cheti cha urithi, kilichoombwa kutoka kwa familia hizi kuthibitisha uhusiano wao na watu waliofariki. Kwa vitambulisho vya kiraia visivyoaminika, mchakato huu unaweza kuchukua miaka kadhaa. Kutokana na hali hiyo, ni familia sita pekee zimepokea msaada wa faranga za CFA milioni 10 hadi sasa…
Ili kuharakisha mchakato huo, masharti yamerahisishwa. Vyeti vya uthibitisho wa urithi havihitajiki tena; uthibitisho wa maombi unatosha, pamoja na cheti cha kifo na jinsia ya mtu aliyefariki. Kisha kuna taratibu za kisheria ili kupata ukweli na haki kuhusu vifo hivi, pamoja na mamia ya kesi zinazodaiwa kuwa za mateso…
Kwa wakati huu, karibu hakuna kesi za kisheria zimeanza. Mapema mwezi Agosti, Waziri wa Sheria aliwasilisha suala hilo kwa mwendesha mashtaka.