Madagascar imekuwa na maadhimisho ya kupokea mafuvu matatu ya watu, yaliyokuwa yamehifadhiwa nchini Ufaransa kwa miaka 128.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mmoja wa fuvu hilo linaaminiwa kuwa ya aliyekuwa Mfalme nchini Madagascar, aliyekatwa kichwa na wanajeshi wa Ufaransa wakati wa kipindi cha ukoloni katika Karne ya 19.
Ufaransa ilirejesha mafuvu hayo kutoka jijini Paris Agosti 27, katika utekelezwaji wa sheria ya kurejesha sehemu za miili ya watu waliouawa wakati wa kipindi cha ukoloni barani Afrika.

Mabaki yaliyorejeshwa nchini Madagascar, yanaaminiwa kuwa ya Mfalme Toera, kiongozi wa kabila la Sakalava, alieyakatwa kichwa pamoja na walinzi wake wawili mwaka 1897, na sehemu zao za miili kupelekwa Ufaransa kama ishara ya ushindi.
Baada ya sehemu hizo wa mwili kurejeshwa, zinatarajiwa kuzikwa katika eneo la Belo Tsiribihina, umbali wa Kilomita 320 kutoka jiji kuu Antananarivo.

Vichwa vyao, vimekuwa vikihifadhiwa katika makavazi ya kihistoria jijini Paris, pamoja na vitu vingine vya kale, vilivyotolewa Madagascar katika kipindi cha miaka 60 ya ukoloni.