Watoto milioni sita wapo kwenye hatari ya kutoenda shuleni mwaka ujao, kufuatia kukatwa kwa fedha za msaada kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNICEF.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

UNICEF kupitia taarifa yake, imeonya kuwa wahisani wanapunguza msaada wa fedha  kuwezesha wanafunzi kutoka nchi masikini hasa Afrika kupata elimu, kwa asilimia 24 ambapo kiwango cha Dola Bilioni 3.2 kitapungua.

Wanafunzi katika nchi za Afrika Magharibi na Kati, ndio wanaotarajiwa kuathiriwa zaidi, ambapo watoto zaidi ya Milioni 1.9 wapo kwenye hatari ya kutorudi shuleni kuanzia mwaka ujao.

Nchi za Cote Dvoire na Mali, zinatajwa kuwa nchi zenye hatari kubwa, ambapo wanafunzi wapatao 340,000 huenda wasiendelee na elimu yao na wengine 180,000 nchini Mali, iwapo wahisani kufikiria upya uamuzi wao, ili kuwawezesha watoto kupata haki ya elimu.

Hii imetokana na hatua ya serikali ya rais wa Marekani chini ya uongozi wa rais Donald Trump, ambao umetangaza kuwa, itapunguza msaada wake wa kigeni kwa Dola Bilioni 3.2 kwa mwaka wa 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *