
Kongamano la siku tatu, kujadili hali ya amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, linaloandaliwa na wakfu wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Thambo Mbeki, limeanza jijini Johannesburg bila ya uwakilishi kutoka upande wa serikali.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waandalizi wa kongamano hili wanasema, linatoa jukwaa kwa makundi mbalimbali nchini DRC kujadiliana kuhusu namna ya kupata amani ya kudumu katika nchi yao.
Wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na wajumbe kutoka upande wa rais wa zamani Joseph Kabila, na viongozi wa dini na wawakilishi wa mashirika ya kiraia, wanashiriki katika mazungumzo hayo, lakini serikaliya rais Felix Tshisekedi imekataa kushiriki.
Uongozi wa M23/AFC chini ya Corneille Nangaa, pia umetuma ujumbe wa watu saba, huku mwanasiasa wa upinzani Jean-Claude Kibala akisema amezuiwa kuondoka jijini Kinshasa, na waalikwe wengine kunyimwa viza.
Siku kadhaa zilizopita, rais Tshisekedi alisema, mazungumzo yanayokubalika ni yale yanayoandaliwa na Wakongamani ambayo yatafanyika nchini humo.
Serikali ya DRC inaonekana kupendelea mchakato wa mazungumzo ya Doha na mkataba wa Washington DC licha ya kuendelea kupata shinikizo za kuandaa mazungumzo ya kitaifa na makundi yote ili kupata mwafaka wa kitaifa.