Mali imetangaza kuwa imewasilisha malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya Algeria, ikiituhumu kwa kudungua ndege isiyo na rubani ya jeshi lake katika ardhi ya Mali mapema mwezi Aprili 2025.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Mvutano unaongezeka tena kati ya Mali na jirani yake, Algeria. Utawala wa kijeshi wa Mali umetangaza katika taarifa yake siku ya Alhamisi kwamba umewasilisha malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya Algeria, ukiituhumu kwa kudungua ndege isiyo na rubani ya jeshi lake katika ardhi ya Mali mapema mwezi Aprili.

Mambo ya Kisheria

Mzozo kati ya nchi hizo mbili sasa unaelekea kwenye uwanja wa kisheria. Tangu Aprili 1, Bamako imeishutumu Algiers kwa kudungua ndege isiyo na rubani ya jeshi la Mali katika eneo la Mali, karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili. Kwa utawala wa kijeshi, kitendo hicho kinajumuisha ukiukaji wa anga yake.

Algeria, kwa upande wake, imefutlia mbali shutuma hizi. Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Algeria, data ya rada iliyokusanywa “inathibitisha wazi ukiukaji wa anga ya Algeria” na ndege ya upelelezi kutoka Mali.

Jambo hilo lilizua mzozo wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, ambazo zinashiriki mpaka wa karibu kilomita 1,500 kwa urefu. Bamako na Algiers wamefunga anga zao kwa kila upande.

Kwa mujibu wa taarifa ya utawala wa kijeshi wa Mali kuwasilisha malalamiko yake mbele ya ICJ, “uchokozi huu wa wazi ni kilele cha mfululizo wa vitendo vya uhasama na unaonyesha wazi ushirikiano usiofaa kati ya magaidi na utawala wa Algeria.”

Kwa waangalizi, malalamiko ya Mali dhidi ya Algeria ni kukanusha majaribio ya hivi punde ya Algiers ya kuboresha uhusiano wake na Bamako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *