Jeshi la Israel limeanza kushambulia majengo marefu kwenye mji wa Gaza, katika operesheni inayosema, inawalenga Hamas.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika wiki za hivi karibuni, wanajeshi wa Israeli wamekuwa wakiendeleza operesheni maalum kuwahamisha wakaazi wa Gaza, hatua ambayo inashtumiwa na Jumuiya ya Kimataifa.

Aidha, jeshi limesema limebaini kuwa majengo hayo marefu yanatumiwa na Hamas kutekeleza mipango yake.

Wakati hayo yakijiri, wanajeshi wa Israeli, wamewauwa watu zaidi ya 40 kwenye ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa, wakiwemo watoto saba.

Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF, limelaani kulengwa kwa watoto, na kuelezea mashambulio yanayoendelea, hayakubaliki.

Wizara ya afya kwenye ukanda wa Gaza, inasema asilimia 30 ya Wapalestina, waliouwa kwenye vita vuta ni watoto.

Watu zaidi ya Elfu 64 wameuawa tangu Israeli ilipoanza operesheni ya kuwasaka Hamas, mwezi Oktoba mwaka 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *