
Waziri Mkuu wa Japan Shigeru Ishiba ametangaza kujiuzulu leo Jumapili, Septemba 7, chini ya mwaka mmoja baada ya kuchukua madaraka. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 68 anajiuzulu chini ya shinikizo linaloongezeka kutoka kwa chama chake, Liberal Democratic Party (LDP), kilichodhoofishwa na matokeo mabaya katika uchaguzi wa maseneta msimu huu wa joto.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Nimeamua kujiuzulu kama mwenyekiti wa chama cha Liberal Democratic Party,” Waziri Mkuu Shigeru Ishiba amesema, akimaanisha chama tawala cha Japan, ambacho kimetawala kwa takriban miongo kadhaa. “Sasa kwa kuwa mazungumzo kuhusu hatua za ushuru wa Marekani yamekamilika, ninaamini ni wakati mwafaka,” amesema, akihalalisha mabadiliko yake ya msimamo wakati wa hotuba yake Jumapili. “Nimeamua kuachia ngazi na kutoa nafasi kwa kizazi kijacho.”
Uamuzi huu haukushangaza, kutokana na shinikizo alilokuwa nalo mkuu wa serikali. Lakini Shigeru Ishiba hadi sasa alikuwa amepuuza wito huu, na kutangaza tena Jumanne kwamba “atafanya uamuzi ufaao wakati utakapofika.”
Baada ya kuingia madarakani mwezi Oktoba 2024 baada ya kuondoka kwa Fumio Kishida, amekosolewa kwa kushindwa mfululizo kwa LDP. Katika uchaguzi wa maseneta mnamo mwezi Julai 20, muungano unaoongozwa na chama chake-kinachoundwa na chama cha kihafidhina cha mrengo wa kulia cha Liberal Democratic Party (LDP) na mshirika wake mkuu Komeito-ulipoteza wingi wake katika baraza hili la juu, miezi michache tu baada ya kuunda serikali ya wachache katika bunge la chini.
Yale ambayo yalikuwa matokeo mabaya zaidi kwa chama chake cha Liberal Democratic katika miaka 15 yamekuwa yasiyoweza kusameheka, na kusababisha chama hicho kupoteza ukiritimba wake wa muda mrefu wa mamlaka, anaripoti mwandishi wetu huko Tokyo, Frédéric Charles.
Kulingana na kituo cha televicheni ya serikali ya Japan, NHK, Waziri Mkuu amependelea kujiuzulu ili kuepusha migawanyiko ya ndani, huku Gazeti la kila siku la Asahi Shimbun likibaini kwamba hangeweza tena kupinga miito iliyokua ya kutaka kuondoka kwake.
Jioni iliyotangulia, Ishiba alikutana na Waziri wa Kilimo Shinjiro Koizumi na Waziri Mkuu wa zamani Yoshihide Suga, ambao walimtaka aondoke wadhifa wake. Siku chache kabla, maafisa wanne waandamizi wa LDP, akiwemo Katibu Mkuu Hiroshi Moriyama, walijitolea kujiuzulu, na kuzidisha udhaifu wa serikali yake.
Hata hivyo, Shigeru Ishiba hahusiki pekee na mzozo huu wa kisiasa unaotokea katika nchi ya Japan inayoonyeshwa kwa muda mrefu kama kielelezo cha utulivu wa kisiasa. Kushindwa kwa chama cha Kidemokrasia cha Liberal kunaweza kuelezewa na watu wa Japan kutokuwa na imani na mfumo wao wa kisiasa. Ufichuzi wa kuwepo kwa “fedha duni” ndani ya chama cha Conservative, ufadhili wa siri wa chama chenyewe, na uhusiano wake na madhehebu ya Umoja wa Kanisa la Mwezi unafichua hali mbaya ya demokrasia ya Japan. Kwa hiyo, karibu nusu ya watu wa Japan hawapigi kura.