Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mwaka wa shule, uliopangwa awali kuanza siku ya Jumatatu, Septemba 1, haukuanza tena katika shule kadhaa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini. Hii ni kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya kundi la AFC/M23 na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na Wazalendo. Hali hiyo inahatarisha mustakabali wa maelfu ya watoto, licha ya kujitolea kwa usitishaji vita kati ya pande hizo mbili ambazo ziko katika mazungumzo mjini Doha.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika mkoa wa Kivu Kaskazini, shule zilizoathiriwa ziko hasa kwenye mpaka kati ya maeneo ya Walikale na Masisi. Katika maeneo hayo, madarasa hayakufunguliwa. Kutokana na hali hiyo ya ukosefu wa usalama, Kaurwa Hilaire, Mkuu wa Shule ya Msingi ya Showa iliyopo Masisi, anaeleza:

“Mwaka wa shule huko Showa, hatujui ni lini utaanza.” Hadi 85% ya watu wametoroka makazi yao huko Maisi; hatutathubutu kufungua milango huko maana bado kuna ukosefu wa usalama. Tunafikiria kufungua shule hapa, Masisi; kwanza tunasubiri idhini kutoka kwa mamlaka.”

Huko Kivu Kusini, maelfu ya wanafunzi pia wameshindwa kurejea shuleni katika eneo la Itombwe eneo la Mwenga. Hii pia ni kutokana na mapigano ya hivi karibuni kati ya waasi na jeshi linaloungwa mkono na Wazalendo.

Elewano Ishimwindulwa Zidane, afisa wa utawala wa eneo hilo, anatoa wito kwa serikali ya Kongo kuchukua hatua kwa maslahi ya elimu ya watoto: “Kuna shule nyingi zilizoathiriwa na mapigano. Na katika shule zote hizi, ziwe za msingi au za sekondari, hakuna hata moja kati ya shule hizo iliyo na wanafunzi chini ya 300. Jaribu kuzidisha idadi hiyo kwa takriban shule 80 ambazo hazijafunguliwa.” 

Kote DRC, zaidi ya wanafunzi milioni 29 wametakiwa kuanza shule wiki hii, kulingana na takwimu rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *