
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye ametangaza serikali mpya jioni ya Jumamosi, Septemba 6, ambapo Mawaziri wa Sheria na Mambo ya Ndani wameondoka na Waziri mpya wa Mambo ya Nje ameteuliwa, kwa mujibu wa agizo lililosomwa kwenye televisheni ya umma.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwanadiplomasia Cheikh Niang, balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa mjini New York na nchi nyingine kadhaa, ndiye Waziri mpya wa Mambo ya Nje wa Senegal. Anachukua nafasi ya Yassine Fall, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Sheria akichukuwa nafasi ya Hakimu Ousmane Diagne, ambaye alikuwa anaongoza wizara hii tangu serikali ya kwanza kuundwa mwezi Aprili 2024. Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ni Mouhamadou Bamba Cissé, wakili wa Waziri Mkuu Ousmane Sonko.
“Hii haitakuwa serikali ya kustarehesha, lakini serikali ya kujitolea na kupambana. Hatutakuwa wachapa kazi na kuwa makini.” “Tutalazimika kufanya kazi saa 24 kwa siku, siku saba kwa wiki, kutokana na hali iliyopo,” ametangaza Waziri Mkuu Ousmane Sonko, akirejelea rekodi ya zamani ya utawala wa rais wa zamani Macky Sall (2012-2024).
Ameelezea mabadiliko katika Wizara ya Sheria kama nia ya idara hiyo “kuboresha maridhiano na raia wa Senegal na kurejesha imani yao.” Waziri Mkuu Sonko na baadhi vigogo wa chama tawala hivi majuzi wamekosoa, hasa, ucheleweshaji, wanasema, katika uchunguzi wa mahakama kuhusu ghasia zilizosababisha vifo vya watu kadhaa kati ya mwaka 2021 na 2024 na utawala uliopita.
Ousmane Sonko ateuliwa tena kuwa Waziri Mkuu
Ousmane Sonko ameteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu na Rais Faye, ambaye aliingia madarakani mwezi Aprili 2024. Ousmane Sonko alimuweka kwenye nafasi yake baada ya kuwania kwake urais katika uchaguzi wa mwezi Machi 2024 kubatilishwa. Timu hiyo mpya inawekwa katika wakati ambapo Senegal inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi, inayoashiria nakisi ya bajeti ya 14% na deni la umma ambalo linawakilisha 119% ya Pato la Taifa. Kiwango cha ukosefu wa ajira kinakadiriwa kuwa 20%, wakati umaskini unafikia 35.7% ya watu, kulingana na takwimu rasmi.
Mapema mwezi Agosti, Waziri Mkuu Sonko alizindua “mpango wa kufufua uchumi na kijamii” unaokusudiwa “90%” kufadhiliwa na rasilimali za ndani ili “kurudisha mamlaka” kwa nchi, ambayo kwa sasa iko kwenye majadiliano na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa msaada zaidi wa kifedha. Mamlaka mpya zinadai kuwa zimerithi mambo mazito, kulingana na mamkala hizo, kutoka kwa Rais wa zamani Macky Sall, ambaye alishutumiwa kwa kuficha takwimu za kweli kwenye viashirio muhimu kama vile deni la umma na nakisi ya bajeti.