Haya ni kwa mujibu wa wizara ya mambo ya kigeniya Poland.

Tangazo hilo linafuatia operesheni iliyofanywa na Umoja wa Ulaya na Poland ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, kuzidungua droni zinazoshukiwa kuwa za Urusi zilizoingia katika anga yake.

Urusi imekanusha kuhusika na tukio hilo, huku mwanadiplomasia mkuu wa Poland akisema droni hizo zilitokea upande wa Ukraine, uliovamiwa na Urusi mwaka 2022.

Hayo yanafanyika wakati ambapo ofisi ya rais wa Ukraine imesema Rais wa Finland Alexander Stubb amewasili nchini humo kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Volodymyr Zelensky.

Inaarifiwa kwamba miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika mkutano wa viongozi hao wawili ni hakikisho la usalama kwa Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *