Ujumbe mkubwa wa serikali kutoka jijini Kinshasa, unatarajiwa mjini Uvira, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia, baada ya kushuhudiwa kwa maandamano yenye vurugu kwa siku kadhaa zilizopita, yaliyopangwa na mashirika ya kiraia na wapiganaji wa Wazalendo, kumkata Jenerali Olivier Gasita kuongoza usalama katika eneo hilo.
