
Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, wiki hii alizuru nchi ya Haiti ambapo ameonya kuhusu kasi ndogo ya msaada wa jumuiya ya kimataifa kwa nchi hiyo kukabiliana na makundi ya majambazi pamoja na hali mbaya ya kibinadamu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tom Fletcher alizuru mji mkuu, Port-au-Prince kutathmini mzozo wa kibinadamu unaozidi kuzorota kutokana na kuenea kwa ghasia za magenge ambayo yameua maelfu ya watu na kuwaacha zaidi ya milioni moja bila makazi.
Akizungumza alipozuru mojawapo ya makazi ya muda ambayo huhifadhi wakimbizi wa ndani takribani milioni 1.3, Fetcher alisema kuwa kinachofanywa kuwasaidia wananchi ni muhimu, lakini bado kuna pengo la msaada.
Afisa huyo alitoa wito mwingine kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati na kuonya kuwa hali itakuwa mbaya sana iwapo fedha za msaada zitaisha mwishoni mwa mwezi.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, magenge hayo karibu yanadhibiti eneo lote la mji mkuu, na mamlaka zimeshindwa kuzuia vurugu katika taifa hilo la Caribbean.