Vifo vya malaria huenda vikaongezeka mwaka huu kutokana na kupunguzwa kwa misaada ya kigeni, mkurugenzi wa taasisi ya Global Fund, yenye makao yake Geneva, ameonya.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Sekta ya afya kwenye mataifa mengi masikini duniani, imetatizika tangu uamuzi wa ghafla wa rais wa Marekani, Donald Trump wa kupunguza ufadhili wa nje wa kifedha.

Wakati nchi nyingine pia tangu wakati huo zimepunguza bajeti zao za misaada ya maendeleo, sekta hiyo imeathiriwa pakubwa ambapo kawaida Marekani ilikuwa mfadhili mkubwa zaidi duniani.

Wataalamu wanasema bara la Afrika ndilo litaathirika pakubwa, ambapo mapambano dhidi ya ugonjwa huo yamekwama katika miaka ya hivi karibuni, kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa migogoro, usugu wa dawa na uhaba wa fedha.

Donald Trump alitangaza kukatisha misaada ya kigeni ambayo ilikuwa inawasaidia watu wengi zaidi duniani.
Donald Trump alitangaza kukatisha misaada ya kigeni ambayo ilikuwa inawasaidia watu wengi zaidi duniani. © Alex Brandon / AP

Ugonjwa wa Malaria, ambao huenezwa na mbu, husababisha vifo vinavyokadiriwa kufikia laki 6 kila mwaka, huku wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano wakifariki kwa wingi.

Kulingana na shirila la Sands, utafiti wa mpango wa Roll Back Malaria unasema kunaweza kuwa na vifo zaidi ya laki 1 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *