Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kwamba nchi yake haina lengo la kuunda silaha za nyuklia. Rais Pezeshkian ametoa hotuba hiyo wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla ya vikwazo vya kimataifa kuanzishwa tena dhidi ya taifa hilo kutokana na shughuli zake za nyuklia.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimechukua hatua ya kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa ambavyo vilikuwa vimesitishwa chini ya mkataba wa nyuklia wa 2015 ambao ulifikiwa na Marekani na kisha kuvunjwa na Rais Donald Trump. Wanadiplomasia wa pande mbili wamekutana kulijadili suala hilo kabla ya vikwazo vinavyotarajiwa kuanza jumamosi. Kiongozi huyo pia amelaani mashambulizi ya Israel na Marekani mnamo mwezi Juni akisema ni pigo kubwa kwa uaminifu wa kimataifa na matarajio ya amani ya kikanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *