Watu 20 wamejeruhiwa, wawili wako katika hali mbaya kutokana na shambulio la droni katika mji wa Eilat kusini mwa Israel. Jeshi la Israel limesema droni hiyo ilitokea Yemen na kuanguka. Hapo baadae waasi wa Kihouthi walidai kuhusika na shambulio hilo wakisema wamefanya operesheni sahihi ya kijeshi kulenga maeneo ya Israel katika mji wa Eilat. Siku ya Jumanne, kitengo cha kijeshi cha Wahouthi kilifanya shambulio jingine kwa kutumia ndege nyingi za droni kuyalenga maeneo ya Israel.

Wanamgambo wa Kihouthi wenye makao yake Yemen wamekuwa wakishambulia mara kwa mara maeneo ya Israel kwa makombora na droni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Israel, ambayo inaendesha vita dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza, imeshambulia maeneo yaliyoko umbali wa kilomita 2,000 nchini Yemen ambayo inasema yanahusishwa na shughuli za kijeshi za Wahouthi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *