Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.9 kipimo cha Richter lililopiga katikati mwa Ufilipino siku ya Jumanne jioni imeongezeka hadi 72, kulingana na shirka la ulinzi wa raia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti iliyotolewa leo Alhamisi na shirika hilo, watu 294 pia walijeruhiwa. Idadi hii mpya ya vifo inawakilisha vifo vingine vya watu watatu siku ya Jumatano, huku waathiriwa wote wakiripotiwa katika eneo la Visayas ya Kati.

Tetemeko hilo la kina kirefu lilipiga maji kutoka kisiwa cha kati cha Cebu katikati ya usiku, na kuharibu nyaya za umeme, madaraja, na majengo mengi, ikiwa ni pamoja na kanisa llililojengwa karne moja iliyopita.

Tetemeko la ardhi la Cebu ndilo baya zaidi kuwahi kuripotiwa nchini humo tangu angalau mwaak 2013, wakati tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.2 kipimo cha Richter lilipiga kisiwa jirani cha Bohol na kuua watu 222.

Ufilipino ambao unapatikana karibu na kile kinachojulikana kama “Pete ya Moto” ya Pasifiki, hukumbwa na matetemeko zaidi ya 800 kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *