Kongamano hilo la siku mbili lililoitishwa na rais wa zamani wa Kongo, Joseph Kabila aliyehukumiwa kifo nchini mwake hivi majuzi, mjini Nairobi, linawaleta pamoja wapinzani kadhaa wa Félix Tshisekedi pamoja na washirika wengi wa karibu wa Joseph Kabila. hata hivyo, viongozi wengi muhimu hawajahudhuria mkutano huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumanne, Oktoba 14, Nairobi, mji mkuu wa Kenya, umekuwa mwenyeji wa mkutano wa siku mbili wa sehemu ya upinzani wa Kongo ulioitishwa na rais wa zamani Joseph Kabila, aliyehukumiwa kifo hivi karibuni na mahakama ya kijeshi ya DRC kwa uhaini na uhalifu dhidi ya amani.

Mkutano huo uliopewa jina la “Kongamano la makundi ya kisiasa na Kijamii kuhusu Mustakabali wa nchi,” unalenga kusikiliza maoni ya kila mtu na kubainisha suluhu zinazowezekana, kwa mujibu wa mshirika wa karibu wa mkuu huyo wa zamani wa nchi.

Wapinzani waliohudhuria ni pamoja na Augustin Matata Ponyo, Waziri Mkuu wa zamani chini ya Joseph Kabila ambaye sasa anaishi uhamishoni baada ya kukutwa na hatia ya ubadhirifu, na Franck Diongo, mkuu wa chama cha Progressive Lumumbist Movement (MLP), ambaye alijitenga na Rais Félix Tshisekedi baada ya kumuunga mkono.

Aliyekuwa mgombea urais aliyekaa gerezani kwa miezi sita kwa kuchochea uasi, Seth Kikuni pia yuko pamoja na wafuasi wakuu wa rais huyo wa zamani, kama vile Barnabé Kikaya Bin Karubi, mmoja wa washauri wake wakuu, na Raymond Tshibanda, mratibu wa chama cha Common Front for the Congo (FCC).

Mkutano wafanyika licha ya kukosekana kwa wahusika kadhaa wakuu wa upinzani

Mkutano huu unafanyika katika mazingira ya mzozo wa kisiasa na kiusalama unaotikisa mashariki mwa DRC na wakati ambapo upinzani unaendelea kutoa wito wa kuwepo kwa mazungumzo jumuishi chini ya upatanishi wa madhehebu ya kidini ili kuutatua.

“Wazo ni kuleta pamoja nguvu muhimu za taifa na kutambua suluhu zinazowezekana, tiba,” anaelezea Patient Sayiba, mshiriki wa karibu wa Joseph Kabila aliyepo Nairobi, ambaye anahoji: “Mgogoro ni mkubwa. Je, tunapaswa kukaa kimya?”

Mkutano huu, hata hivyo, unafanyika wakati viongozi kadhaa wakuu wa upinzani wa Kongo, kama vile Moise Katumbi, Delly Sesanga, na Jean-Marc Kabund, hawakushiriki. Kuhusu Martin Fayulu, hakualikwa, kwa mujibu wa msemaji wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *