
Chanzo cha picha, Israeli foreign ministry
Jeshi la
wanamaji la Israel limekamata meli zilizokuwa zimebeba misaada kuelekea Gaza na
kuwaweka kizuizini wanaharakati waliokuwa ndani, akiwemo mwanaharakati wa hali
ya hewa wa Uswidi Greta Thunberg.
Wizara ya
Mambo ya Nje ya Israel ilisema meli kadhaa ambazo ni sehemu ya Global Sumud
Flotilla (GSF) “zimesimamishwa kwa usalama” na kwamba zinaelekezwa
hadi katika bandari ya Israel.
Iliongeza
kuwa jeshi la wanamaji liliambia meli hizo kubadili mkondo kwa kuwa “zinakaribia eneo la mapigano”.
GSF
ilielezea uvamizi huo kama “kinyume cha sheria” na “si kitendo
cha kujilinda” bali ni “kitendo cha unyanyasaji “.
Pia unaweza kusoma: