#HABARI: Katika jitihada za kukuza Sekta ya Madini na kuongeza mchango wake katika pato la Taifa, wachimbaji na wachenjuaji wadogo wa dhahabu wilayani Songwe, wamezindua mitambo ya kisasa ya kuchenjulia madini yenye thamani ya shilingi bilioni moja nukta tatu.
Mitambo hiyo, ambayo imesimikwa katika kijiji cha kimborokoto, imewekwa na kampuni ya uchenjuaji madini ya njabu kwa lengo la kuongeza thamani ya madini ya dhahabu pamoja na kuhifadhi mazingira kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, katibu wa kampuni ya njabu, Bw. Joshua Dongwala, alisema uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata fursa ya kusindika madini yao kwa ufanisi na kwa viwango vya kitaifa huku Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Kumbuka Njabu, aliishukuru serikali kwa mazingira bora ya uwekezaji na kuomba msaada zaidi wa kitaalam na kifedha ili waweze kupanua zaidi huduma zao.
Uwekezaji huo umeivutia serikali ambapo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ndg. Ismail Ali Ussi, amefika kujionea maendeleo hayo akiwa na ujumbe wake. Akizungumza baada ya uzinduzi Ussi amewawapongeza wawekezaji hao wazawa kwa ubunifu na ujasiri wao nakuongeza kuwa mradi huo ni chanzo cha ajira kwa wakazi wa eneo hilo kwani unasaidia kuchangia ukuaji wa uchumi wa wilaya ya songwe kupitia ushuru na kodi mbalimbali.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.