Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendeleza misingi ya amani, umoja na haki huku akiongoza nchi kwa utu na uadilifu mkubwa.

Akizungumza leo, Oktoba 7, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Sengerema mkoani Mwanza, Makonda amesema uongozi wa Dkt. Samia umejikita katika upendo na usawa kwa Watanzania wote bila ubaguzi, jambo linaloendelea kuimarisha mshikamano wa kitaifa.

✍ Mwandishi Wetu
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *