
Katika kulipiza kisasi kwa vikwazo vilivyowekwa na Beijing kwenye sekta ya kimkakati ya juu ya ardhi adimu, Donald Trump ametangaza kwenye mtandao wake wa Truth Social kwamba Marekani itatoza ushuru mpya wa 100% kwa bidhaa za China, pamoja na ule ambao tayari unatumika, kuanzia Novemba 1 “au kabla.”
Imechapishwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Makabiliano kati ya Trump na Beijing yamezuka tena na tangazo hili la ushuru mpya kwa bidhaa za China. Bilionea huyo wa chama cha Republican, akielezea kwamba alikuwa akijibu “mkao wa kibiashara wenye uchokozi wa kupita kiasi” uliopitishwa na nchi hiyo ya pili kwa ukubwa duniani, pia amebainisha kwamba vikwazo vya usafirishaji wa “programu zote za kimkakati” kwenda China vitatumika tarehe hiyo ya Novemba 1.
Donald Trump alitangaza siku ya Ijumaa, Oktoba 10, pia kwenye jukwaa lake la Truth Social, kwamba “hakuna tena sababu yoyote halali” ya kukutana na mwenzake wa China Xi Jinping kama ilivyopangwa katika wiki mbili, kutokana na mtazamo wa “uhasama uliokkthiri” wa China.
Trump apatwa na hasira, soko la hisa linaporomoka
China, nchi ambayo inaongoza duniani kwa uzalishaji wa ardhi adimu, nyenzo muhimu kwa tasnia, na Washington ilikuwa tayari imeishutumu kwa kutumia vibaya nafasi hii kuu. Udhibiti mpya uliotangazwa siku ya Alhamisi na Beijing unahusu usafirishaji wa teknolojia zinazohusiana na uchimbaji na utengenezaji wa nyenzo hizi, kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Biashara ya China. “Huu ulikuwa mshangao wa kweli,” amekiri rais wa Marekani. “Nilitakiwa kukutana na Rais Xi baada ya wiki mbili kwenye mkutano wa kilele wa APEC (Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki) huko Korea Kusini, lakini inaonekana hakuna sababu tena” ya kufanya hivyo, kiongozi huyo kutoka chama cha Republican ameongeza.
Soko la Hisa la New York limelemewa na kuanza tena kwa uhasama huo, ambao unahitimisha kipindi cha utulivu kati ya Beijing na Washington. Lilifungwa kwa kasi, hata kabla ya rais wa Marekani kutangaza ushuru wa ziada. Wastani wa Viwanda wa Dow Jones umepungua kwa 1.90%, faharisi ya Nasdaq ilishuka 3.56%, na faharisi pana ya S&P 500 imepoteza 2.71%, ikifuta faida zake zote kutoka kwa wiki mbili zilizopita.
“Hakuna jinsi China itaruhusiwa kushikilia ulimwengu mateka, lakini hiyo inaonekana kuwa mpango wao kwa muda,” Donald Trump amesema.
Uhusiano wa kibiashara kati ya China na Marekani, ambao umepata misukosuko mwaka 2025, umekuwa na hali ya utulivu katika wiki za hivi karibuni. Mnamo mwezi Septemba, Donald Trump alikuwa na mazungumzo na Xi Jinping ambayo yalielezewa kuwa “ya tija,” mazungumzo yake ya tatu tangu mwanzo wa mwaka. Akiwa ameridhika na mijadala kuhusu suala jingine nyeti sana, yaani mustakabali wa jukwaa la TikTok nchini Marekani, alitaja hata safari ya China mwaka ujao, pamoja na ziara ya mwenzake nchini Marekani.
Katika mzozo mwingine wa kibiashara, China ilitangaza siku ya Ijumaa kwamba itaweka majukumu “maalum” kwa meli za Marekani kwenye bandari zake, kulipiza kisasi kwa hatua kama hizo zilizochukuliwa na Washington mnamo mwezi Aprili. Marekani, kwa upande wake, ilisema imeondoa “mamilioni” ya bidhaa zilizopigwa marufuku za Wachina kutoka kwa majukwaa ya biashara ya mtandaoni.
Chini ya mashambulizi ya ulinzi yaliyoanzishwa na Donald Trump tangu kurejea kwake madarakani Januari 20, ushuru wa forodha kati ya nchi hizo mbili umefikia viwango vya juu mara tatu kuliko kawaida kwa pande zote mbili, na kuvuruga mitandao ya ugavi. Hata hivyo, Washington na Beijing zilifikia makubaliano yenye lengo la kupunguza mvutano, kupunguza kwa muda ushuru hadi asilimia 30 kwa bidhaa za China zinazoingizwa Marekani na hadi 10% kwa bidhaa za Marekani zinazoingizwa China.
Makubaliano ya kibiashara ambayo yaliporomoka siku ya Ijumaa yalipaswa kudumu hadi Novemba 10.