Jeshi la Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo linatoa wito kwa waasi wa FDLR, wanaochukuliwa na Kigali kuwa “tishio lililopo,” kuweka chini silaha zao, kifungu muhimu cha makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi Juni kati ya majirani hao wawili chini ya upatanishi wa Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Kongo Sylvain Ekenge ametoa wito kwa kundi la waasi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), kilichoundwa na viongozi wa zamani wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, kujisalimisha “kwa nia ya kuwarejesha katika nchi yao ya asili,” katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, Oktoba 10.

Mashariki mwa DRC, eneo lenye utajiri wa maliasili na linalopakana na Rwanda, limekuwa likikumbwa na migogoro kwa miaka thelathini.

Ghasia zimeongezeka tangu mwezi Januari na kutekwa kwa miji mikubwa ya Goma na Bukavu na kundi linaloipinga serikali la M23, linaloungwa mkono na Kigali na jeshi lake (RDF).

Mwishoni mwa mwezi Juni mjini Washington, DRC na Rwanda zilitia saini mkataba wa amani ambao haukumaliza ghasia.

Rwanda inahalalisha uungaji mkono wake kwa M23 kwa kuwepo kwa katika maeneo ya mashariki mwa DRC waasi wa kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), kundi lenye silaha lililoanzishwa na viongozi wa zamani wa Kihutu wa Rwanda wa mauaji ya kimbari ya Watutsi 1994 na kuchukuliwa na Rwanda kuwa “tishio lililopo.”

Siku ya Ijumaa, jeshi la Kongo lilitoa wito kwa “makundi yote” ya FDLR “kuweka silaha zao chini na kujisalimisha kwa mamlaka ya Kongo au MONUSCO kwa nia ya kuwarejesha katika nchi yao ya asili, Rwanda,” katika taarifa iliyotiwa saini na msemaji wake, Sylvain Ekenge. Uamuzi huu ulichukuliwa “kama sehemu ya” utekelezaji wa makubaliano ya Washington, jeshi limesema, bila kutaja masharti au ratiba ya upokonyaji silaha wowote unaowezekana.

“Katika tukio la upinzani na kukataa kutii,” vikosi vya Kongo “vitapokonya silaha kwa kulazimishwa au kutumia nguvu,” taarifa inaongeza.

Mkataba wa amani uliotiwa saini mjini Washington mwezi Juni unatoa fursa ya kupokonywa silaha kwa FDLR na wanamgambo wengine, pamoja na kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Kongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *