
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, siku ya Ijumaa, Oktoba 10, ameamua kumteua tena Sébastien Lecornu kama Waziri Mkuu. Mfuasi huyu mwaminifu wa Rais wa Jamhuri, ambaye alijiuzulu mapema wiki hii huku kukiwa na ukosefu wa kuungwa mkono na vyama vya mrengo wa kulia vikiahidi kupinga, amekabidhiwa tena wadhifa wa Waziri Mkuu. Chaguo hatari kwa Emmanuel Macron, kwani upinzani ulikuwa tayari umetangaza nia yao ya kupinga serikali.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waziri Mkuu Sébastien Lecornu, alitangaza Oktoba 8, baada ya kumalizika kwa mashauriano yake, kwamba Waziri Mkuu mpya atateuliwa na Emmanuel Macron ndani ya saa 48. Muda wa mwisho ulimalizika siku ya Ijumaa, Oktoba 10. Na jioni hiyo, Rais Emmanuel Macron alimteua tena Sébastien Lecornu kuwa Waziri Mkuu.
Siku nzima, Rais Emmanuel Macron alikutana na viongozi wa vyama mbalimbali, ispokuwa viongozi wa vyama vya Rassemblement national na La France Insoumise. Kwa mujibu wa wasaidizi wa Rais Emmanul Macron, vyama hivi viwili vya siasa havikualikwa kwa sababu “vilionyesha kwamba vinataka kuvunjwa” kwa Bunge.
Kuteuliwa tena kwa Sébastien Lecornu hakuungwi mkono na mrengo wa kushoto au mrengo wa kulia wenye msimamo mkali. Akiwa ameteuliwa kwa shida, vyama vya La France Insoumise na Rassemblement national vilitangaza kwamba vitaipinga serikali ya Waziri Mkuu.
Katika mkutano uliofanyika Ijumaa jioni, idadi kubwa ya wabunge wa Les Républicains walionyesha kumuunga mkono Sébastien Lecornu. Chama cha Kisoshalisti, kwa upande mwingine, kilionya kwamba kitampinga Waziri Mkuu bila “kusitishwa mara moja na kamili” kwa mageuzi ya pensheni.