Nchini Ufaransa, Sebastien Lecornu, aliyeteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu, anaendelea kupata shinikizo za kisiasa, kuhakikisha anapata bajeti itakayoungwa mkono na pande zote.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati Lecornu, akipata shinikizo hizo, vyama vya siasa vinatishia kuwasilisha bungeni mswada wa kukosa imani naye, baada ya kujiuzulu siku chache zilizopita na kuteuliwa tena kwenye nafasi hiyo.

Hatua ya rais Macron kumteua tena kwenye nafasi hiyo, kumesababisha mvutano mkubwa wa kisiasa, licha ya Lecornu, siku ya Jumamosi kuahidi, kuwateuwa Mawaziri ambao hawajafungwa na vyama vyao vya siasa.

Aidha, ameahidi kushirikiana na vyama vyote vya siasa, ili kupata bajeti itakayosaidia kupambana na ongezeko la deni la taifa.

Lecornu, anatarajiwa kuwasilisha  mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2026, kufikia siku Jumatatu.

Wanasiasa kutoka chama cha Kisholisti, wanasema hawana maelewano na Lecornu kuhusu mipango ya uundwaji wa serikali mpya.
Wanasiasa kutoka chama cha Kisholisti, wanasema hawana maelewano na Lecornu kuhusu mipango ya uundwaji wa serikali mpya. REUTERS – Stephanie Lecocq

Aliyekuwa Waziri wa usalama Bruno Retailleau, amewaambia wanasiasa wake wa chama cha Republicans, kuwa hawatashiriki kwenye serikali mpya itakayoundwa.

Wanasiasa kutoka chama cha Kisholisti, wanasema hawana maelewano na Lecornu kuhusu mipango ya uundwaji wa serikali mpya.

Chama cha mrengo wa kulia cha National Rally, kinachoongozwa na Jordan Bardella, kinasema hakina mpango wowote wa kuingia kwenye serikali mpya na badala yake, itawasilisha mswada wa kukosa imani na Sebastien Lecornu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *