Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Bin Zubeir Ally, amewataka Waislamu na Watanzania kwa ujumla kulinda amani na mshikamano wa taifa, hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza na waumini wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, Mufti amesema amani ndiyo msingi wa Uislamu na chachu ya maendeleo, akisisitiza malezi ya watoto katika misingi ya dini ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *