#HABARI: Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025 hadi 2030, katika Jimbo la Peramiho kimeahidi kuiunganisha Tanzania na Msumbiji kwa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 122, kutoka eneo la Likuyufusi kupitia Mkayukayu hadi mpaka wa Mkenda.

Hayo yamesemwa na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Peramiho Bi. Jenista Mhagama, wakati akinadi sera za CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya chama hicho katika Kijiji cha Nakawale Kata ya Muhukuru.

Amesema fursa nyinginezo za kiuchumi ambazo zitaambatana na ujenzi wa barabara hiyo ni ujenzi wa soko kubwa la kimataifa katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.

Bi.Mhagama amewataka wananchi kuchangamkia fursa zitakazoambatana na ujenzi wa barabara hiyo pamoja na soko kubwa la kimataifa kwa kuanza mapema maandalizi ya kupokea miradi hiyo na kushiriki kikamilifu katika maendeleo yatakayoletwa na Serikali ya CCM.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *