Abiria zaidi ya 700 wa treni ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma kupitia reli ya kati, hatimaye wameendelea tena safari yao baada wahandisi wa TRC kukamilisha ukarabati wa reli.
Taarifa kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC) zinaeleza kuwa kuchelewa huko kulitokana na ajali ya treni ya matengenezo iliyotokea katika eneo la Kintiku, mkoani Singida, na kusababisha uharibifu wa kipande cha reli.
Awali, Meneja wa Stesheni ya Dodoma, Festo Mgomapayo, alisema abiria hao walifika Dodoma majira ya saa 2 usiku Oktoba 14, na kuendelea na safari saa 8 mchana Oktoba 15, mara baada ya wahandisi wa TRC kukamilisha ukarabati wa reli na kuruhusu safari kuendelea kwa usalama.
✍ Ahmady Ally Mramba
#AzamTVUpdates