Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wameuelezea mkutano wa Sharm al-Sheikh kuwa ni onyesho la nguvu na hadaa zenye lengo la kupuuza haki za watu wa Palestina.

Mwenendo wa dharau na kudhalilisha ya Rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano wa hivi karibuni wa Sharm al-Sheikh nchini Misri na viongozi wa eneo, mkabala wa usitishaji vita aliotwishwa yeye na Waziri Mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu na Muqawama wa Kiislamu wa Palestina, Hamas na wananchi wa Gaza, imeugeuza mkutano huo kuwa jukwaa la mafunzo ya kihistoria.

Kwa mujibu wa Pars Today, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X waliuona mkutano wa kilele wa Sharm el-Sheikh kama onyesho la udanganyifu ambapo haki za watu wa Palestina zilisahauliwa waziwazi.

Kuhusiana na hili, mtumiaji wa mtandao wa kijamii wa X anayeitwa “Tawana Rafiei” aliandika: “Zogo la Sharm al-Sheikh, Misri lilikuwa ni jaribio la kushawishi maoni ya umma. “Maonyesho ya dharau na kutafuta madaraka yalianza katika Bunge la Israel “Knesset” na kufikia Sharm el-Sheikh. Haki zisizoweza kuondolewa za watu wa Palestina zilipuuzwa tena.”

Mtumiaji mwingine wa X, Sreejit Datta, aliandika: “Baada ya kutazama onyesho la Sharm al-Sheikh, ni lazima mtu aketi nyuma kwa tabasamu la hasira na kutazama picha ya ukumbusho ya washiriki ambao walikanyaga kwa urahisi haki halali za Wapalestina.”

Hamid Tariq pia alisema: “Wale wanaojiita watetezi wa amani ambao walikusanyika Sharm al-Sheikh “kukomesha” mauaji ya halaiki huko Gaza hawaogopi vita, bali uhuru wa taifa ambalo silaha yake pekee ni muqawama.”

Mwanaharakati mwingine wa X, Mohammad Reza Najafi, aliandika: “Trump na Netanyahu muuaji watoto, pamoja na watumishi wao huko Sharm el-Sheikh, walikuwa wakitafuta kitu ambacho hawawezi kuchukua kutoka kwa muqawama wa Gaza baada ya miaka miwili ya vita.”

“Mahdi” pia alisisitiza: “Katika mkutano wa kilele wa Sharm al-Sheikh, Trump muuaji aliwafedhehesha na kuwakejeli wafuasi wake wote kwa kadiri alivyoweza, ili wote wajue kwamba wao si chochote zaidi ya chombo cha kudharauliwa, lakini jambo la muhimu zaidi ni kwamba muqawama sio wa kudharauliwa, na hawawezi kuwapokonya silaha Hamas wala kuwafedhehesha watu wa Palestina.”

Mustafa Babajani pia aliufananisha mkutano wa kilele wa Sharm el-Sheikh na ngome ya wanyama na akaandika: “Katika ngome hii, damu inachuruzika kutoka kwenye mikono ya wauaji wa watoto wa Gaza.”

“Hossein Marouf” pia anaamini: “Ulimwengu ulishuhudia tukio la kushtua na la kipuuzi zaidi la kisiasa katika karne iliyopita. Maonyesho katika Knesset ya Israel na Sharm al-Sheikh, Misri, yalikuwa kilele cha uchafua wa kisiasa. Uigizaji safi wa ucheshi wa Donald Trump, na mkabala wake leo nimegundua jinsi watu wa Palestina walivyosimama kidete na kuendesha muqawama kwa ustadi.”

“Gohari” pia alisema: “Mkutano wa kipuuzi zaidi wa makubaliano ya amani duniani ulifanyika Sharm al-Sheikh. Mkutano ambao Trump alikuja kama kichekesho kikubwa kupeana mikono na wakuu wa nchi na kuondoka. Heshima hii ilikuwa muhimu kwake baada ya kushindwa kwake kupata Tuzo ya Amani ya Nobel.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *