Mradi wa miaka mitano wa utambuzi wa magonjwa ya mlipuko umekamilisha awamu yake ya kwanza, ukilenga magonjwa ya Dengue na Chikungunya.

Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii (NPHL), Ambele Mwafulango, amesema mradi huo uliofadhiliwa na Taasisi ya Kofih ya Korea, unalenga kuimarisha uwezo wa maabara nchini katika kutambua magonjwa kwa haraka na kutoa majibu sahihi kwa usalama wa jamii.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali kuimarisha mifumo ya afya, licha ya changamoto ya matumizi holela ya dawa bila vipimo miongoni mwa wananchi.

✍ Tumie Omary
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *