#HABARI: Katika tukio la kugusa hisia nyumbani kwa familia ya Hayati Raila Odinga, binti yake Winnie Odinga alionekana akimkabidhi mama yake kofia maarufu ya ‘White Fedora’ aliyokuwa akiivaa mara kwa mara baba yao mpendwa.

Kofia hiyo imekuwa ishara ya utambulisho wa Raila katika mikutano na shughuli mbalimbali za kisiasa. Kukabidhiwa kwa mama yao kumetafsiriwa kama alama ya heshima, upendo, na urithi wa maisha ya uongozi na mapambano ya kisiasa aliyoyaacha.

Tukio hilo lilitokea mara baada ya mwili wa Raila kuwasili nyumbani, na limegusa wengi waliokuwa wakifuatilia tukio hilo, wakiona ishara ya mshikamano wa kifamilia na njia ya kipekee ya kumuaga mpendwa wao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *