Serikali ya Kenya imetangaza Ijumaa ya Oktoba 17, 2025 kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya, Raila Amolo Odinga, aliyefariki dunia jana nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Tangazo hilo limetolewa kupitia Gazeti la Serikali Na. 15007 chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Likizo ya Umma (Sura ya 110), ambapo Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, Kipchumba Murkomen, alithibitisha uamuzi huo kwa niaba ya serikali.
Mazishi ya kitaifa ya kiongozi huyo yamepangwa kufanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi siku ya Ijumaa, ambapo viongozi wa ndani na wa kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria kutoa heshima zao za mwisho.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi