Nchini Tanzania, kampeni za uchaguzi zinafanyika katika hali ya wasiwasi inayozidi kuongezeka. Wiki mbili kabla ya uchaguzi wa Oktoba 29, visa vya watu kukamatwa na kutoweka vinaongezeka. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni watu wengi wamekamatwa na hawajulikani waliko, ikiwa ni pamoja na balozi wa zamani Cuba, Humphrey Polepole, kada wa zamani wa chama tawala na mkosoaji wa utawala. Kipindi hiki kinashuhudia mabadiliko makubwa kwa ukandamizaji. Wakati tume ya uchaguzi ikichora upya ramani ya nchi, Mahakama Kuu imekata kumuidhinisha mgombea watatu katika kinyang’anyiro hicho.

Mabaki ya damu yaliyokutwa chini, mlango ulivunjwa, kamera za uchunguzi kuzimwa kabla ya shambulio… Jijini Dar es Salaam, kupotea kwa aliyekuwa balozi Humphrey Polepole kumeshangaza wengi nchi Tanzania na nje ya nchi hiyo. Kulingana na familia yake, kada huyo wa zamani wa chama tawala, ambaye amekuwa mkosoaji wa utawala, alitekwa nyara kutoka nyumbani kwake usiku wa Jumatatu, Oktoba 6.

Polisi wanasema wanachunguza, lakini hawajatoa matokeo yoyote. Leo, ukandamizaji huo unaenea nchi nzima na walengwa sio wale wa upinzani, na katika kambi ya chama tawala wanalengwa kwa sasa, anaelezea wakili William Maduhu. “Wanachama wa chama cha siasa cha CCM sasa ndio walengwa wa ukandamizaji. Chama tawala pengine kilifikiri kuwa utekaji nyara huu ungewagusa wanaharakati tu au wapinzani. Lakini ikiwa balozi wa zamani anaweza kutekwa, hebu fikiria nini kinaweza kutokea kwa mwananchi wa kawaida? Visa hivi vya watu kutoweka vilianza chini ya utawala wa John Magufuli, lakini hapana kwa kiwango hiki. Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa zamani wa serikali kulengwa,” anaeleza.

Watetezi wa haki za binadamu sasa wanahofia kutokea kwa ghasia

Hali ya ni ya wasiwasi zaidi tangu tume ya uchaguzi ilipofuta maeneo kumi ya bunge na kuhamisha vituo kadhaa vya kupigia kura. Hatua hii inachukuliwa na upinzani kuwa inatia shaka. Na siku ya Jumatano, Mahakama Kuu ilikataa kuidhinisha mgombea huyo wa ACT Wazalendo, chama cha tatu kwa ukubwa kisiasa, kwa uamuzi kwamba haiwezi kuingilia maamuzi ya tume ya uchaguzi ambayo tayari ilikuwa imemkataa kwa makosa ya kiutawala.

Kutokana na hali hiyo, CCM, chama cha Rais Samia Suluhu Hassan, kinajikuta kikiwa peke yake katika kinyang’anyiro hicho. Na zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya uchaguzi, watetezi wa haki za binadamu sasa wanahofia kutokea kwa ghasia Oktoba 29.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *