Mjane aliyeamriwa kuondoka katika nyumba anayoisimamia akiwa masimamizi wa mirathi ya marehemu mumewe iliyopo Msasani Dar es Salaam, Alice Haule amerejeshewa hati ya nyumba hiyo baada ya tume iliyoundwa kwa lengo la kuchunguza uhalali wa mauziano ya eneo ilipo nyumba hiyo kubaini kuwa mke wa marehemu hajathibitika kusaini nyaraka za mkopo wa fedha.
Mkopo huo unadaiwa kuchukuliwa na marehemu mumewe kabla ya kifo chake ndio uliosababisha Alice na watoto wake waamriwe kuondoka na kuiacha nyumba hiyo kwa anayedai kuwa mkopeshaji wa fedha kwa marehemu.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi