Mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la watu duniani ni miongoni mwa mambo yanayotishia kupelekea kuzuka tena kwa  ugonjwa huo wa Malaria  unaoweza kusababisha kifo. Ukosefu wa fedha za kutosha kwa ajili ya mipango yenye gharama kubwa ya kuzuia kuenea kwa malaria, unahatarisha juhudi dhidi ya ugonjwa huo unaoenezwa na mbu na hivyo kuyaweka hatarini maisha ya mamia kwa maelfu ya watu.

Muungano wa Viongozi wa Afrika dhidi ya Malaria (ALMA) na mashirika mengine yameeleza katika ripoti mpya kuwa athari hizo zitashuhudiwa zaidi barani Afrika ambako kunaripotiwa asilimia 95 ya visa vya ugonjwa huo ambao ulisababisha vifo 590,000 kote duniani mnamo mwaka 2023.

Hata hivyo ripoti hiyo imebainisha kuwa vifo vitokanavyo na Malaria vimepungua kwa nusu katika miongo miwili iliyopita. Aidha, Novemba 21 kutafanyika mkutano nchini AfÅ•ika Kusini ili kujaribu  kukusanya michango  itakayoelekezwa katika Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *