Rais Samia, alitumia takribani dakika 30 kuelezea namna serikali ya chama chake tawala cha CCM ilivyowezesha maendeleo hasa katika jiji la Dar es Salaam.

Mgombea huyo ameyazungumza hayo katika mkutano huo wa kwanza wa kampeni uliokutanisha wilaya za Ubungo na Kinondoni akijinadi kuwa chama chake kimefanya mapinduzi makubwa kwa jiji hili ambalo mwenyewe ameliita ndio Tanzania yenyewe.

Kadhalika mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya CCM, amesema endapo chama chake kitapata ridhaa basi watakamilisha ujenzi wa miundombinuikiwamo kuongeza bajeti ya miradi ya barabara.

Amewaahidi wakazi wa Dar es Salaam kuwa kuanzia Januari, 2026 kutakuwa na mageuzi makubwa ya utoaji wa huduma ya miundombinu ya mwendokasi.

Wafuasi wa CCM katika mkutano wa kampeni jijini Dar es Salaam
Chama tawala cha CCM kinatazamiwa kushinda uchaguzi mkuu kwa kishindo baada ya chama kikuu cha upinzani kufunguiwa kushirikiPicha: Florence Majani/DW

Rais Samia amesema serikali itaendelea kusimamia haki na usawa kwa watu wanaoishi na ulemavu kwa kuendelea kutekeleza matamko ya kimataifa ya kutomwacha mtu nyuma.

Alihitimisha hotuba yake akiwasisitiza Watanzania waende kupiga kura, akisema kuwa maandamano pekee yatakayokuwepo ni ya watu kwenda kupiga kura. Kadhalika alitumia wasaa huo akisema matusi na kejeli zote abebeshwe yeye kwa kuwa aliapa kuitumikia Tanzania.

Akizungumzia karata hii ya turufu katika dakika za lala salama kwa CCM, mchambuzi wa masuala ya siasa kutoka Shule ya Sayansi ya Sasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Abel Kinyondo amesema.

Miongoni mwa waliohudhuria kampeni hizo na kupata wasaa wa kuzungumza, ni Ezekiel Wenje, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA Kanda ya Victoria ambaye hivi karibuni amehamia rasmi CCM. Wengine waliohudhuria mkutano huo wa kampeni ni mawaziri wa wizara mbalimbali, wagombea ubunge kwenye majimbo ya Ubungo, wake za marais wastaafu, na viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *