Mgombea Ubunge Jimbo la Handeni Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Reuben Kwagilwa, ameahidi kuhakikisha wananchi wa…Mgombea Ubunge Jimbo la Handeni Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Reuben Kwagilwa, ameahidi kuhakikisha wananchi wa…

Mgombea Ubunge Jimbo la Handeni Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Reuben Kwagilwa, ameahidi kuhakikisha wananchi wa Handeni wanapata huduma ya maji safi na salama ndani ya kipindi cha miezi minne, endapo atapewa ridhaa ya kuongoza tena katika awamu inayofuata.

Kwagilwa ametoa ahadi hiyo wakati akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Oktoba 22,2025, katika Kata ya Chanika, Wilaya ya Handeni Mjini, mkutano ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama, akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdalah.

Akizungumza mbele ya wakazi wa kata hiyo, Kwagilwa amesema tatizo la maji limekuwa likiwakabili wakazi wa Handeni kwa muda mrefu, na kwamba kwa kutumia uzoefu alionao pamoja na kushirikiana na mamlaka husika, atahakikisha changamoto hiyo inapata suluhisho la haraka.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdalah, aliwataka wananchi wa Handeni Mjini kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi na kuwachagua wagombea wa CCM, akisisitiza kuwa chama hicho kina sera madhubuti na viongozi wenye nia ya dhati ya kuwatumikia

#StarTvUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *