
Seyyed Abbas Araqchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, sharti la kurejea Iran katika meza ya mazungumzo ni Wamarekani kucha siasa zao za kijuba na za kupenda makuu.
Abbas Araghchi ameeleza kuuwa, mazungumzo ambayo yalikuwa yakiendelea na Marekani, pamoja na mazungumzo ya New York, yalisitishwa na hayakuendelea kutokana na ujuba wa Marekani na tabia yake ya kuupenda makuu.
Araghchi alisema kwamba simu na jumbe zilitumwa kwa Steve Witkoff, Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani katika Masuala ya Mashariki ya Kati (Asia Magharibi), kupitia mpatanishi, na akasema: “Tumeonyesha kwamba siku zote tumejitolea kutatua masuala ya kidiplomasia, lakini hii haimaanishi kuwa ni kuondosha haki za watu wa Iran. Popote pale ambapo maslahi ya watu wa Iran na maslahi makuu ya nchi yanaweza kupatikana kwa njia ya diplomasia, tulichhukua hatua lakini tulikuumbana na watuu ambao katu hawajawahi kuheshimu diplomasia.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliongeza: “Maadamu moyo huu, mtazamo, na uzoefu wa uchungu katika mazungumzo na Wamarekani upo, ni jambo la kawaida kwamba hakuna uwezekano wa kuingia tena mazungumzo isipokuwa kama njia ya Wamarekani itabadilika na wakafikia natija kwamba mazungumzo yana msingi wa kuheshimiana na misimamo sawa.”
Araqchi aliongeza: “Wamejaribu njia nyingine na hawajapata matokeo, na ikiwa wataendelea na mchakato huo tena, bado hawatapata matokeo wanayotarajia.”