Wakazi wa vijiji vya Kasahanga na Buzimbwe vilivyopo wilayani Bunda mkoani Mara wameishukuru serikali kwa ujenzi wa vizimba maalumu vinavyowaruhusu kuchota maji katika Ziwa Victoria bila kuwa katika hatari ya kushambuliwa na mamba.
Vizimba hivyo vimejengwa na serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini TAWA.
Imeandaliwa na Rebeca Mbembela