
Komoro imewasilisha tamko rasmi la kujiunga na kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Israel iliyofunguliwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).
Kwa kujibu wa taarifa ya ICJ, tarehe 29 Oktoba 2025, Komoro ikitumia kifungu cha 63 cha Kanuni ya Mahakama, iliwasilisha katika Daftar la Mahakama tamko la kuingilia kati katika kesi inyaohusu Utekelezaji iwa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza (Afrika Kusini dhidi ya Israel).
Afrika Kusini iliwasilisha kesi hiyo mwezi Disemba 2023 ikiituhumu Israel kwa mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza. Tangu wakati huo, mataifa kadhaa yamejiunga na mchakato huo wa kisheria zikiwemo Uhispania, Ireland, Libya, Mexico, Ubelgiji na Uturuki.
Mahakama ya ICJ imewasilisha hatua tatu za muda ikiiamuru Israel izuie vitendo vya mauaji ya kimbari na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.
Zaidi ya Wapalestina 68,000 wameuawa Gaza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili ya mashambulizi ya Israel tangu Oktoba mwaka 2023.
Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas yalifikiwa tarehe 10 Oktoba kwa msingi wa mpango wa amani wa vipengele 20 uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump. Hata hivyo utawala wa Israel umekiuka makubaliano hayo mara kadhaa hadi sasa.