
Kuanzia Guinea hadi mashariki mwa Kongo, mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari yanazidi kuwa makubwa kote barani Afrika, na kutokujali kunaendelea hata kama wahalifu mara nyingi wanajulikana.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku hii ilianzishwa mahsusi na umoja wa Mataifa, kuwakumbuka waandishi wawili wa habari wa idhaa ya RFI, Ghislaine Dupont na Claude Verlon, ambao waliuawa Novemba 2 mwaka 2013 wakiwa katika majukumu yao kaskazini mwa nchi ya Mali kwenye mji wa Kidal, baada ya kutekwa na wanajihadi wa kiislamu.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Pamoja na ofisi ya haki za binadamu ya umoja wa Afrika, kwa Pamoja wameonya kuhusu wanahabri kunyamazishwa, kutishwa n ahata kuuawa wanapotekeleza majukumu yao.
Kufuatia ongezeko la mauaji ya wanahabari, wadau wanataka mataifa kuweka mikakati ya kuwalinda, ikiwemo kutunga sheria ambazo zitahakikisha uhuru wa vyombo vya habari barani Afrika.
David Omwoyo ni mwenyekiti wa baraza la wanahabari duniani na pia mkurugenzi wa baraza la wanahabari nchini Kenya, MCK.
Kwingineko picha ya mwahabari Serge Oulon inaonekana kwenye ukurasa wa mbele wa Gazeti la L’Evènement, tangu mwezi Julai 2024, gazeti maarufu nchini Burkina Faso, linamsubiri mhariri mkuu wake arudi kabla ya kuonekana tena.
Asubuhi ya Juni 24, 2024, kundi la watu wenye silaha lilivamia nyumba ya mwandishi huyo aliyebobea katika uchunguzi na kumpeleka mahali pasipojulikana.
Watu wengine kadhaa mashuhuri katika vyombo vya habari vya Burkina Faso walitekwa katika mazigira kama hayo miezi iliyofuata.
Baada ya kutwaa madaraka katika mapinduzi mwishoni mwa mwaka 2022, utawala wa Kapteni Ibrahim Traoré umekuwa hauna uvumilivu tena na watu wanaojaribu kukosoa utawala wake. Ni “waandishi wa habari wazalendo” pekee wanaoruhusiwa kufanya kazi zao”, gazeti hilo linaandika.