Mkataba huo utaonesha kuwa ushirikiano wa Marekani na Uingereza unasalia kuwa imara licha ya tofauti kuhusu mizozo ya Ukraine, Mashariki ya kati na pia kuhusu mustakabali wa miungano ya nchi za Magharibi.

Trump kwanza atakutana na Mfalme Charles III katika kasri lake Windsor, kisha baadaye atakutana na Waziri Mkuu Keir Starmer.

Miongoni mwa mikataba inayotarajiwa kusainiwa wakati wa ziara ya Trump ni pamoja na utakaoharakisha miradi mipya ya nyuklia na kile maafisa wa Uingereza wamekiita “ushirikiano wa kiteknolojia wa hali ya juu duniani”.

Kabla ya ziara hii, kampuni ya Google ilitangaza kuwa itawekeza pauni bilioni 5 nchini Uingereza katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Nayo kampuni za kifedha za Marekani kama PayPal na Citi Group zilitangaza uwekezaji wa pauni bilioni 1.25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *