#HABARI: Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu, amewataka wadau wanaoendesha Vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, Makao ya Watoto na Nyumba Salama nchini kuwekeza katika malezi ya Watoto kupitia huduma wanazotoa.
Dkt. Jingu ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Kongamano lililowakutanisha Umoja wa Wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo mchana, Makao ya Watoto na Nyumba Salama ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Ustawi wa Jamii katika Viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama Dar Es Salaam.
Amewataka wamiliki hao kuzingatia Sheria, taratibu na Kanuni za uendeshaji wa Vituo hivyo huku akisisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya uzalendo kwa watoto ili kujenga Jamii yenye ari na kuipenda nchi yao.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania