HUYU HAPA KOCHA MSAIDIZI: “Nina furaha kuwa kwenye hii timu”
Kocha mpya msaidizi wa Yanga SC, Patrick Mabedi amesema ana furaha kujiunga na timu hiyo kwasababu vijana hao wa Jangwani wana mipango mikubwa na yeye anapenda timu zenye mipango kama hiyo.
Kocha huyo amesema Yanga ina historia kubwa na ina wafuasi wengi na ameiona timu hiyo ikifanya vizuri.
Kwa upande wake Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, ashusha sifa za kocha huyo huku akifunguka kuhusu kocha msaidizi aliyekuja na Kocha Romain Folz.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#YangaSC