IRAN vs TANZANIA: “Tuna changamoto kwenye safu ya ushambuliaji”
Mchambuzi wa soka @akingamkono anasema kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kina safu nzuri ya ulinzi na ndio maana kwenye takwimu za mechi tano zilizopita, Stars haijafungwa magoli mengi.
Kingamkono anasema shida ipo kwenye safu ya ushambuliaji na hapo Kocha Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’ ana kazi ya kukinoa vema kikosi chake ili kiweze kutengeneza magoli.
Taifa Stars leo itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wao Iran na mechi itakuwa LIVE #AzamSports1HD saa 12:00 jioni.
Kwa upande wake mchambuzi @adrianojames_ anasema tatizo la washambuliaji limekuwa ni kama la taifa zima.
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#Viwanjani