Kansela Merz wiki iliyopita alisema kuwa visa vya uhalifu katika miji mikuu ya Ujerumani vinatokana na ongezeko la wahamiaji.

Alipoulizwa na mwandishi mmoja alichomaanisha kuhusu matamshi yake hayo, kansela huyo alimwambia mwandishi huyo awaulize “wanawe wa kike” kama anao.

Na sasa mbunge katika bunge la Ulaya ambaye pia ni mkuu wa masuala ya kijamii katika chama cha Merz cha CDU, Dennis Radtke, amejitokeza na kudai kuwa kama kansela, Merz ana jukumu la kuleta uwiano wa kijamii.

Matamshi ya Merz pia yamekosolewa na chama cha kisoshalisti cha SPD ambacho ni chama kilicho katika serikali ya muungano pamoja na CDU, huku Katibu wake Mkuu Tim Kluessendorf, akisema Merz anapanda mbegu za migawanyiko na kuvunja uaminifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *