Rais Masoud Pezeshkian amewasilisha rasmi sheria ya kujiunga Iran na Mkataba wa Kimataifa wa Kupambanana Ufadhili wa Ugaidi (CFT).

Katika barua yake siku ya Jumanne, Pezeshkian aliziarifu taasisi husika kuhusu sheria iliyoidhinisha ya kujiunga Iran na mkataba huo. 

Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tarehe Mosi Oktoba ilipasisha kwa masharti kujiunga Iran na mkataba wa Kimataifa wa Kupambana na Ufadhili wa Ugaidi (CFT).

Mohsen Dehnavi, Msemaji wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametaja masharti yaliyoainishwa na Iran kwa ajili ya kujiunga na mkataba huo, na kueleza kuwa Bunge lilieleza kuwa kufungamana Iran na masharti ya mkataba huo kutakuwa katika fremu  ya Katiba ya nchi. 

The Financial Action Task Force kwa kifupi (FATF), ambao ni muungano wa kimataifa wa kupambana na utakatishaji fedha haramu na kufadhili vitendo vya ugaidi wenye makao yake makuu Paris, Ufaransa, mwaka 2020 uliiorodhesha Iran baada ya kuidhinisha Azimio la Palermo na Mkataba wa CFT.  

Wizara ya Fedha ya Iran pia imeeleza kuwa kikozi kazi kwa jina la The Financial Action Task Force (FATF) huwenda kikajadili katika mikutano yake ijayo suala la kujiunga Iran na mkataba wa Kimataifa na Kupambana na Ufadhili wa Ugaidi (CFT).

Iran inakabiliwa na vikwazo vya upande mmoja vya Marekani vinavyosababisha mazingira magumu kwa nchi hii kuwa na uhusiano wa kawaida wa kibenki na kifedha na nchi nyingine duniani. 

Weledi wa masuala ya uchumi pia wanasema kuwa Iran inapasa kuondolewa katika orodha nyeusi ya FATF ili nchi hii iweze kudumisha uhusiano wake wa kibiashara  na nchi zinazopinga sera za vikwazo za Umoja wa Mataifa na Marekani dhidi ya Tehran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *