
Katika ulimwengu wa biashara, kampuni ya saruji ya China ya Huaxin imepata mafanikio ya kimkakati nchini Nigeria. Imenunua mitambo kadhaa ya saruji kutoka kwa kampuni ya Uswisi kwa dola bilioni 1. Hii inaiweka kampuni ya China moja kwa moja katika nafasi ya tatu kati ya kampuni kubwa zaidi za saruji nchini, nyuma ya mabilionea Aliko Dangoté na Abdul Samad Rabiu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa kupata hisa za kampuni ya Uswisi ya Holcim kutoka Lafarge Africa nchini Nigeria, kampuni ya China ya Huaxin imepata mitambo minne ya saruji yenye uwezo wa kuzalisha tani milioni 10 kwa mwaka. Huu ni ushindani mkubwa dhidi ya kampuni za saruji za Nigeria.
Hii inatoa ushindani mkubwa kwa bilionea Aliko Dangoté, ambaye kampuni yake ni kampuni namba moja ya saruji katika bara la Afrika. Soko kubwa la Nigeria ni jengo jingine la Huaxin Cement barani Afrika.
Mkakati wazi na wa haraka wa upanuzi
Mnamo mwaka wa 2020, kulikuwa na ununuzi wa kitengo cha kwanza nchini Tanzania, kisha ununuzi wa kampuni ya Ufaransa Lafarge nchini Zambia na Malawi, kabla ya Zimbabwe na Afrika Kusini.
Kutokana na kukabiliwa na soko la mali isiyohamishika ambayo inakwenda kwa mwendo wa kinyonga nchini China, kamapuni kama Huaxin zinatafuta maduka mapya ya vifaa vyao vya ujenzi, na Afrika ndio soko la kwanza linalolengwa.
Huaxin Cement sasa inazalisha tani milioni 30 kwa mwaka katika nchi kumi katika bara hili, ikikaribia kwa karibu tani milioni 52 zinazozalishwa na kampuni ya Dangote Cement.