Huku zikiwa zimesalia chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi wa urais nchini Malawi, kampeni zinaendelea kwa utulivu, lakini katikati ya mgogoro wa kiuchumi. Rais wa sasa Lazarus Chakwera anawania kuchaguliwa tena. Wanaomkabili ni makamu wake wa rais na wakuu wawili wa zamani wa nchi: Peter Mutharika, 85, ambaye kuchaguliwa kwake tena mwaka 2019 kulibatilishwa kutokana na udanganyifu, na Joyce Banda, rais wa kwanza mwanamke nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Huu ni uchaguzi wa hatari kubwa kwa nchi iliyokumbwa na mfumuko wa bei, ufisadi, na shinikizo kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa.

Kwa Wamalawi wengi wanasema suala la kweli katika uchaguzi wa urais wa Septemba 16, 2025, sio kujhuwa nani atashinda, lakini jinsi ya kuishi. Bei ya mfuko wa mahindi, chakula cha msingi nchini Malawi, imeongezeka mara sita katika miaka minne, kutoka kwacha (fedha za Malawi) 10,000 hadi 60,000, sawa na euro 5 hadi 35, wakati wastani wa mshahara ni karibu kwacha 100,000. Mtu anawezaje kununua gunia la mahindi kulisha watoto wake wawili na kulipa kodi? “Haiwezekani,” anashutumu mwanahistoria John Lwanda.

Ili kuweka sawa hali ya mambo, wapiga kura wana chaguo kati ya vyama viwili vikuu. MCP, chama tawala cha Malawi Congress Party na DPP, chama cha upinzani cha Democratic Progressive Party. Pande hizo mbili ambazo zilikuwa mahasimu mnamo mwaka 2019, sasa zinakabiliwa na shutuma zile zile za ufisadi na utawala duni. Wakati huu, DPP inaweza kurejea, si kwa kuungwa mkono, lakini “kupitia kukataliwa kwa chama tawala,” kulingana na mwanahistoria John Lwanda. Ni “chaguo la Hobson,” chaguo lisilo na mbadala halisi, anasema.

“Lakini matatizo yatatokea hasa baada ya uchaguzi, katika muktadha wa kukithiri kwa mfumuko wa bei na shinikizo kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF),” anaonya Crispin Mphande, PhD katika Chuo Kikuu cha Mzuzu nchini Malawi. Anabainisha kushuka kwa thamani ya sarafu inayodaiwa na IMF kungesababisha bei kupanda na hali hiyo inaweza kusababisha kuzuka kwa maandamano ikiwa ahadi za kupunguza bei hazitatekelezwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *