Volker Turk, Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Haki za Binadamu, amelaani hatua ya uongozi wa kijeshi nchini Mali, kuahirisha uchaguzi na kuendelea kuwakamata wapinzani na viongozi wa mashirika ya kiraia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Turk, amesema hali ya Haki za Binadamu katika taifa hilo la Afrika Magharibi, inaendelea kuwa mbaya, miaka mitano tangu jeshi lilipofanya mapinduzi na kuchukua madaraka kwa nguvu.
Mwezi Mei, uongozi wa kjeshi ulitangaza kusimamisha shughulli zote za kisiasa na kupiga marufuku vyama vyote vya siasa.
Kiongozi wa kijeshi Jenerali Assimi Goita mwezi Julai, alitangaza kuendelea kuwa madarakani kwa miaka mitano na kuendelea kuongoza mara nyingi zaidi.

Umoja wa Mataifa unasema, hali hii inafifisha kabisa demokrasia nchini Mali, na kukiuka haki za kila raia, kushiriki kwenye masuala ya nchi yao hasa linapokuja kwenye suala la kupiga kura, na kuamua viongozi wao.
Mbali na changamoto za kisiasa, Mali pia imeendelea kushuhudia utovu wa usalama kutokana na uwepo wa makundi ya kijihadi yanayoshirikina na makundi ya Al-Qaeda na Islamic State.